Ilikuaje: Niliimba nyimbo lakini hazikuwa zinanipendeza - Kush Tracey

Teresia Ndoti Wambui anayefahamika kama Kush Tracey ni msanii ambaye anajulikana na mashabiki na wananchi wengi. Hapo awali, Kush Tracey alikuwa msanii wa nyimbo zisizo za injili.

Alijulikana sana kwa wimbo wake wa 'Huwezi ni dandia' mapema mwaka huu aliweza kubadilisha nia yake na kuokoka na kuanza kuimba nyimbo za injili.

Nilikuwa naimba nyimbo lakini hisia na mawazo yangu hayakuwa katika nyimbi hizo, si kuzipenda sana licha ya mashabiki na watu wengi kuzipenda. Zili nijengea jina lakini moyo wangu haukuwa hapo licha ya nyimbo zangu kutambaa sana,.

Nilkuwa naambia watu siku moja nitakuja kuokoka na pia nitaweza kuimba nyimbo za injili ili niweze kubadilisha maisha ya watu wengi. Alisema Kush.

Msanii Kush Tracey aliweza kuokoka mapema mwaka huu huku akiwashangaza wengi kwa hatua ambayo aliweza kuchukua na kuokoka.

Nilikuwa nimeamua kutoka moyoni mwangu kuwa nitaokoka, kwa maana mambo ambayo nilikuwa nafanya kama kulewa sana nilihukumika moyoni mwangu. Baada ya kuokoka sikuweza kuficha bali niliandika katika mtandao wangu wa kijamii kuwa nimeokoka.

Aliongeza:

Niliokoka kwa maana wasichana wengi wa umri mdogo walikuwa wananiambia kuwa wanapendezwa na mimi na kuwa mimi ni mfano mwema kwao.

Ni maneno ambayo yalinipa uzito mwingi moyoni nikaweza kujiuliza kama mimi ni mfano mwema kwa maisha ya wasichana na hata siimbi nyimbo za mungu.

Kwanini nisibadilike na kuwa mfano mwema kwa njia ifaayo, niliamua nitaweza kubadilisha maisha ya wasichana wengi kupitia nyimbo za injili na si nyimba ambazo hazifai.

Sikua nataka mtu yeyote aige mwenendo wangu ambao nilikuwa nao." Kush alieleza.

Kush alisema kuwa alikuwa mpole tangu utotoni mwake kwa hivo wazazi wake walipomuona ameanza usanii waliweza kushtuka sana kwa maana walimjua kama mtoto mpole, mtulivu na asiyekuwa na maneno mingi.

"Mama yangu alikuwa ananisisitiza kuwa nyimbo ambazo nilikuwa naimba hazikuwa zinanistahili." Aliongeza Tracey.