ILIKUAJE: Nilipoteza kidole changu nikitafuta utajiri - Nelson Namanda

Bwana Nelson Namanda ndiye aliyekuwa mgeni wetu katika kitengo cha Ilikuaje.

Bwana Namanda alisimulia jinsi alivyojipata katika dini la kishetani al maarufu 'Cult' huku akiwa na miaka kumi na minne pekee.

Baba huyu wa mtoto mmoja,  alifunguka jinsi nyanya mmoja alimuingiza katika ile dini na kazi yake ilikuwa kuvuruga huduma za mungu, alikuwa anafanya vile kwa kulala na wanawake wa kanisa. Baada ya kulala na wasichana wale, upendo wao kwa mungu ulikuwa unadidimia.

 "Nina ushuhuda ambao unaanza 2017. Babangu alikuwa anafanya kazi Nakuru kabla ya kurudi Western baada ya kupata stroke na nikapelekwa shule ya huko mashinani.

Nilipofika darasa la sita ndipo mambo yalibadilika kwani siku moja nikielekea kuchota maji baada ya shule, nilipatana na nyanya amebeba pot na amevaa nguo nyeupe juu hadi chini. Akanishika mkono na kusema 'Wewe ni wetu' na sikuchukulia kama kitu kikuu.

Siku hiyo jioni mwili wake ulianza kumwasha na akashindwa kula, kitu saa nane alijipata mahala pale pale alipokutana na yule nyanya na alipojipata mahala pale alipata zaidi ya watu 100 ambao walikuwa wamevalia nguo nyeusi na vitambaa vyekundu.

Dakika kama mbili hivi nyoka mkubwa aliyekuwa na shanga ya dhahabu shingoni akatokea.

Nilipoamka nilihisi mwili ulikuwa umechoka kabisa na sikuwa naweza kufanya chochote. Kitu cha kushtua ni kuwa hamna yeyote katika familia yake ambaye alijua.

Nilikuwa nimepewa mshipi fulani ambao kama ningetaka msichana yeyote hangewahi nikataa na kila ninapo lala na mwanamke, huduma kati yake na mungu inaisha. Nilikuwa nalipwa kuharibu huduma ya mungu.

Anasema alikuwa analipwa 40,000 kila mara alipokuwa anavuruga huduma ya mungu na zile fedha hazikuwa zinamsaidia. Fedha zilikuwa tu za mavazi, pombe na wasichana.

Kuna siku walisema kuwa wamenisaidia sana na sasa walitaka kitu kutoka kwangu wakisema wanataka chochote kutoka mwilini mwangu.

Kwa sababu ya ile tamaa nikaona nisipotoa nitakuwa pabaya, hapo nikaamua kutoa kidole na mwanzo umeamua kutoa chochote huwa sherehe kwao.

Ile siku tunavalia mavazi meupe na nikafungwa macho na kitambaa chekundu na sikuwa na uwoga kwani ile roho ilikuwa inanionesha nafanya jambo njema, hapo kifaa kikali kikapita na kidole changu.

Damu ilipotiririka ile nyoka inakuja na kunywa ile damu.

Anasema baada ya kukatwa kile kidole alipata nguvu za kulala na wanawake kama wanne kila siku na isitoshe alilala na mwalimu wake wa darasa la nane.

Nilitumwa Kesha nihakikishe kuwa hakuna chochote kinaendelea. Nilipofika kwa mlango kitu kinanisukuma nje na wale watu walikuwa wananiambia kuwa nafaa nifanye ile kazi kwani walikuwa wamenilipa.

Nilianguka na kuzirai kwa lisali moja na nilipoamka nikajipata nikiwa Athi River na huko nikajipata kanisa fulani. Yule mhubiri alikuwa anaombea watu huku alikuwa anadanganya watu.

Baada ya kuwacha yale maneno siku moja nikijaribu kuomba nilikuwa napigwa makofi lakini miaka mitano baadaye nimeuona mkono wa bwana.