Ilikuaje: 'Nilishiriki ngono mara ya kwanza nikiwa 39,' nabii Stephen Thuranira

nabii.thuranira
nabii.thuranira
Nabii Stephen Thuranira alishangaza wengi alipofichua kuwa alishiriki ngono kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miaka 39.

Akizungumzia katika kitengo cha Ilikuaje na Massawe Japanni, Thuranira alisema kuwa mapenzi yake yalikuwa kufunga pingu za maisha akiwa 26, ila mungu hakumruhusu.

Sauti ya mungu ilinishawishi nisioe na hapo nikamuuliza mungu mbona na akaniambia kuwa ana kazi kuu nami.

Maishani mwangu sikuwa nimegusa mwanamke yeyote na baada ya kupigana na mungu vita vikuu akaniambia nimchukue Milcah nikiwa na miaka 39. Stephen alisema.

Milcah naye alisema,

Mume wangu wa miaka mingi alikuwa ananipiga na kunitishia na hapo niliamua kutoka kwa ndoa hiyo baada ya kuvumilia sana.

Wawili hawa walipatana mwaka mmoja uliopita huku Milcah akiwa na watoto watatu na anasema kuwa aliitika mwito wa bwana na kuolewa na bwana Stephen.

Utotoni mwa Thuranira, aliwahi kimbia nyumbani na kwenda kuishi kichakani na wanyama, akidai ulikuwa wito wa mungu.

Aliongeza akisema kuwa kule kichakani kazi ilikuwa tu kusoma bibilia na kuimba hafi ikafika wakati wanyama waliana kumzoea na wakaanza kuketi karibu naye.

Sauti ilinituma nikaishi kwa kichaka kwa mwaka mmoja nikiwa na umri wa miaka 18. Hapo babangu aliposkia hilo akauza shamba ili nimalize shule huko Narok.

Kutoka hapo nilikuwa tu napenda kuitanishwa na mungu usiku na mchana.

Anasema safari yake ya unabii ilianza akiwa mchanga kwani alikuwa akioneshwa vitu kwa ndoto, vitu au mambo ambayo yalikuwa yanatendeka siku kadhaa baadaye.

Mwaka wa 2012 ndio nilianza kuona ndoto na kila ndoto zilikuwa zinatendeka. Hii ndege ya Ethiopia iliyoanguka bwana alininenea na nilienda nikiwaambia wakenya watubu. Stephen alisema.

Anasema pia Tsunami iliyotokea Indonesia alikuwa ameoneshwa usingizini na baada ya siku mbili ikatendeka na kuua watu wengi.