pierraandmassawe

Ilikuaje: Niliwachana na baba wa mtoto wangu kabla ya kujua nina uja uzito – Pierra Makena

Dj Pierra Makena ni mama wa mtoto mmoja, akiwa katika mahojiano na mtangazaji Massawe Japanni alisema kuwa amelelewa katika familia ya kikristo licha ya kuwa DJ.

DJ Makena alianza uigizaji akiwa na miaka 17 akiwa katika shule ya upili, pia ni msanii wa nyimbo huku akiwa ameigiza katika vipindi mbambali.

Ilikuaje: Tulikaa na mke wangu kwa miaka 5 bila kupata mtoto – Raila Junior

“Nikiwa nasoma nilikuwa nataka kuwa daktari, lakini siku moja niliweza kukujiwa shuleni na waigizaji wa KBC,

“Walitaka niende nikaigize mwalimu mkuu aliweza kuwapigia wazazi wangu simu wakakubali, nilienda na kipendezwa sana kuwa mtangazaji.” Alisimulia DJ Pierra.

pierraainblue
Kenyan DJ Pierra Makena. PIC Courtesy Instagram

Makena ni mtoto wa nne katika familia ya watoto sita – wavulana watatu na wasichana watatu.

Baadaye aliweza kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume ambaye ni baba wa mtoto wake. Makena alisema kuwa walipendana sana na hata aliweza kufurahi sana akiwa katika uhusiano huo.

Ilikuaje: Rahab Nyawira asimulia vile alikuwa mwizi wa mabavu

“Tulipendana sana na baba wa mtoto wangu, nilifurahi  sana nikiwa katika uhusiano huo kwa sababu nilikuwa napewa chochote nilitaka,

“Ilifika wakati tukakosana na mpenzi wangu, na sikujua ama nilikuwa na mimba, baada ya wiki mbili nilienda hospitali na kuambia kuwa nina ujauzito,

“Ni jambo ambalo liliweza kunipa shida za mawazi hadi nikaweza kukonda na kuwa na mawazo mengi,

“Si kuweza kumshikilia baba wa mtoto wangu kama kupe, ni kwa sababu alikuwa ameshikana na kazi yake kwa hivo nilianza kujifunza kuishi bila yeye,

“Nilikuwa nashindwa nitaanzia wapi kuambia wazazi wangu kwa maana walikuwa wamenilea katika njia ya kikristo.” Alisema Pierra.

pierrainred
Dj Pierra Makena

Wakati familia yake walipoona kuwa DJ Pierra yuko na matatizo ya kimawazo dada yake aliweza kumchukua na kukaa na yeye kwa mawaidha.

I have a girlfriend not a wife! Eric Omondi says after losing Man United bet

Alisema kuwa walikuwa wamepanga wapate mtoto na mpenzi wake bali hakuwa anatarajia haraka hivi aweze kuwa na ujauzito.

“Nilieza kumuambia baba wa mtoto wangu kuwa nina mimba yake na akakubali, nilishtuka sana kwa maana sikua natarajia akubali matokeo,

“Ndio tuliweza kuwa na mipango kuwa tutaweza kupata watoto na yeye, nilishtuka sana nilipopata nina momba licha ya kuwa na mipango tuwe na watoto,

“Kumpata mtoto wangu ni jambo ambalo nzuri sana ambalo halijawahi tendeka maishani mwangu.”Alizungumza Pierra.

Pierra alisema kuwa alichukua muda ili aweze kuendelea na maisha, na anamfurahi mpenzi wake popote pahali alipo akiwa anaendelea na maisha yake.

Photo Credits: instagram/pierramakenaofficial

Read More:

Comments

comments