ILIKUAJE: Nilizaliwa bila mfuko wa uzazi na figo moja - Julian Peter

julian peter
julian peter
Mwanadada kwa jina Julian peter, ndiye aliyekuwa mgeni wetu katika kitengo cha Ilikuaje akihojiwa na Massawe Japanni.

Story yake Julian ni spesheli sana kwani alizaliwa bila mfuko wa uzazi, njia ya uzazi na figo moja. Kulingana naye, hali hiyo ni ugonjwa unaojulikana kama (MRKH) Mayer-Rokitansky-Küster-Hauser.

Julian alizaliwa kwa familia ya watoto wawili wa kike na dadake sasa hivi ameolewa na amejaliwa na familia.

Julian ambaye ni mwalimu, ni mchangamfu na hali yake haijamuangusha au kumshusha moyo kadri na jinsi wengi wangedhania.

Kulingana na Julian, yuko kwenye kikundi cha wanadada 30 humu nchini walio na hali kama yake.

Unajihisi aje kama mwanamke?

Mimi niko salama kabisa, maisha yangu ni ya kawaida kama mwanamke yeyote ila siwezi pata damu yangu ya mwezi kwani sina mfuko wa uzazi, hiyo tu ndio tofauti yangu na wanawake wengine.

Je unaweza shiriki ngono?

Baada ya kufanyiwa upasuaji unaweza shiriki mapenzi kwani italingana na wakati umepona na pia unapaswa kuwa tayari kiakili. Kumbuka umewekwa au umetengenezwa njia ya uzazi.

Ungependa kuolewa?

Mungu akipenda nitaolewa. Lakini sasa hivi niko tayari kupata mtoto kupitia adoption.

Ushawahi jipata ukijihurumia?

Nilijua miaka 12 iliyopita na nilijihurumia kwa mda mchache na baadaye nikaendelea na maisha ya kawaida. Baada ya shule nikafanya utafiti kuhusu hali hiyo na nikajikubali kwani singebadilisha.

Kuna watu ambao hawajui kuhusu jambo hili ila liko ni watu hawajitokezi kuzungumzia, na wanadhani umerogwa.

Anawashauri wanawake wenzake walio na hali kama yake kutojihisi ni kama wako pekee yao na kuwashauri wajitokeze na waungane na kundi lao.