Ilikuaje: Nilizaliwa kijana lakini sasa mimi ni mwanamke - Audrey Mbugua

Audrew Mbugua alizaliwa kama kijana kwa jina Andrew Mbugua kabla ya kubadilisha jinsia yake na kuwa mwanamke, kwa jina Audrey Mbugua.

Akizungumzia katika kitengo cha Ilikuaje naye Massawe Japanni, Audrey alifichua kuwa alihisi kuwa kuwa yeye sio kijana alipokuwa na miaka 19 baada ya kubadilisha tabia.

Alisema kuwa jambo hili halikuchukuliwa kwa urahisi na wazazi wake na ilibidi wamshikilie babake ambaye karibu azirai alipopokea habari.

"Nilizaliwa kama Andrew Mbugua na nikakuzwa kama kijana na ikafika wakati nikahisi kuwa mimi sio kijana. Na nikiwa na umri wa miaka 19 nilianza kubadilisha tabia kwani hisia zangu zilikuwa za msichana. " Alisema Audrey.

Aliongeza,

Sikumwambia mtu kwani pia mimi sikuwa naelewa na niliona nikaambia mtu nikama kuua kisha kujishtaki kwa mtu, niliishi na zile fikra kivyangu. Baada ya miaka miwili nikamwambia rafiki yangu Maseno na alicheka hadi kulia.

Je wazazi walipokea zile habari aje?

Wakati babangu alijua, karibu azirai na tulimshikilia na mamangu aliambiwa baadaye na lakini sijui alipokelea ajezile habari. Mimi na baba yangu tulikuwa na uhusiano mzuri wa karibu.

Sahii uhusiano sio mbaya kama wakati huo na huwa ngumu lakini wakati mwingine tukizungumza ananizungumzia kama kijana wala sio mwanadada, lakini naelewa.

Audrey alielezea kuwa kwa watu wanao geuza jinsia, kuna zile mikakati ambazo hufuatwa na madaktari na isitoshe, kuna tofauti ya dawa anazo meza na  kuna zile steps wanafaa kutumia na madak.

Baadhi ya mikakati inayofuatwa ni upasuaji.

Upasuaji wa kutoa kiungo cha uume haukufua dafu kwani daktari mkuu wa hospitali hiyo aliifutilia mbali shughuli hiyo akidai kuwa nahitaji ruhusa kutoka kwa wazazi.

Wakati huo nilikuwa na miaka 25 kwa hivyo sihitaji ruhusa ya wazazi.

Kitambulisho chake chaonesha yeye ni Audrew Mbugua lakini stakabadhi zake za usafiri zaonesha yeye ni mwanaume kwani amekuwa na shida hadi kwa duka za Mpesa.

Anasema akisafiri kwa uwanja wa ndege yeye huulizwa maswali mengi lakini inambidi amevumilia kwani anaelewa lazima awe mvumilivu.