Ilikuaje: Nilizaliwa na kaka na dada, Musa Ingosi asimulia

Musa Ingosi alizaliwa na wazazi ambao walikua ndugu na dada
Musa Ingosi alizaliwa na wazazi ambao walikua ndugu na dada
Musa Ingosi ni mwanaume  ambaye alizaliwa na mwanamke ambaye aliweza kuwa na uja uzito wa  ndugu yake. Baada ya kuzaliwa, mama yake mzazi aliweza kuambiwa kuwa ameweza kuzaa mtoto wake kwa njia ambaye si halali.

Baada ya kuzaliwa, mama yake pia aliweza kuimizwa amtupe kwa maana alikuwa amekataliwa katika familia.

Mama ya Musa hakuweza kumtupa bali aliweza kupelekwa na rafiki yake akaenda kumuuza kwa shillingi mia 700,

Mama aliniuza kwa shillingi mia saba kwa mama ambaye amenilea, nakunipa masomo hadi darasa la nane,"Aliongea Musa.

Musa aliweza kuuzwa akiwa na miezi nne licha ya kuwa alikuwa mdogo sana na alikuwa anategemea matiti tu ya mama yake, mama ambaye aliweza kumlea aliweza kufariki kwa bahati mbaya.

Alisema kuwa alipofariki aliweza pia kumuachia mama mwingine na kisha akaanza kumtesa.

"Mama yangu alipofariki niliweza kuachwa na ndugu ya mama huyo ambaye alininunua, na kuanza kunitesa, walipokuwa wakila pamoja walikuwa wananitenga,

"Lakini mjomba wangu alinipenda sana ilhali bibi yake aliweza kunichukia kwa maana alijua hadithi yangu," Musa alieleza.

Baada ya muda usiokuwa mrefu, aliweza kutoroka na kuja kuishi mitaani kaunti ya Nairobi, mwaka wa 2002 aliyekuwa kuwa rais wa Kenya rais Mwai Kibaki aliweza kuchukua vijana waliokuwa mitaani kisha akawaingiza katika sekta ya NYS.

Musa alikuwa miongoni mwa vijana yaani chokora waliochukuliwa.

"Mwaka wa 2002 rais Mwai Kibaki aliweza kuchukua vijana wa mitaani na kuwapeleka NYS, niliweza kusomea udereva wa tingatinga kisha nikamaliza,

"Sijawahi ona mama yangu ama kwa kifupi sijawahi ona watu wa jamii yangu," Alisema Musa.

Aliweza kusema kuwa angetamani  sana kumuona mama yake hii ni baada ya mke wake kujifungua mtoto msichana ambaye alimpea hamu ya kumuona mama yake mzazi.

Aliweza kujua hadithi yake angali mtoto "Wenye walikuwa wanaishi na mimi walikuwa wanasema kwa lugha ya mama kuwa mimi ni mtoto ambaye ame laaniwa na hatakikani katika familia,

"Nafahamu familia ya mke wangu kama familia yangu kwa maana sina familia yeyote," Alizungumza Musa.

Aliweza kusema kuwa ataweza kumtafuta mama yake licha ya kuwa mama yake anajua mahali alipo, aliongezea na kusema kuwa siku ile ataweza kumuona mama yake atafurahi sana.

Lakini kwa nini mama yake wala si baba? Alisimulia kuwa mama yake licha ya kuambiwa na familia aweze kuavya mimba, alikataa na kumzaa na hakuweza kumtupa ilhali alimuuza tu.

Pia alisema ana mshukuru Mungu kwa maana ametoka mbali na kumpa mama yake nguvu ya kumzaa baada ya mateso ambayo alipitia.