Ilikuaje: Nimemaliza miaka 14 na siku 14 bila dawa za kulevya - Chris Mwangi

chris maina
chris maina
Mgeni wetu katika kitengo cha ilikuaje ni Chris Mwangi ambaye anasherehekea kufikisha miaka 14 na siku 14 bila kunywa pombe wala kutumia madawa ya kulevya.

Kulingana na Mwangi, alijipata ametumbukia katika mtego ule kwa miaka ishirini ambayo pia alijipata akifanya wizi ili kukimu mahitaji yake ya madawa na pombe na isitoshe alikuwa anywa mafuta ya ndege.

Cha kushangaza ni kuwa alianza kutumia dawa za kulevya na pombe akiwa na umri wa miaka kumi na misita.

Je ni nini ilimpelekea kutumia dawa za kulevya?

Nikikumbuka, nilipomaliza darasa la nane pale Uhuru estate primary school nikapata alama 425/600 nikaitwa shuke ya Pumwani.

Nilitaka kutambulika na ile peer pressure nikajipata niko ndani ya madawa lakini ule ulikuwa ugonjwa wa kurithi (hereditary).

Aliongeza.

Nilianza na bangi kwa sababu nilikuwa na train boxing na mabingwa walikuwa wanavuta sasa nikawaenzi ili niwe kama hao. Iliendelea na nikaanza kupiga cham (chang'aa) na hapo ndio mambo iliharibika na nikaanza kutumia dawa ya diazepam 5 ambayo ni dawa ya upasuaji.

Halafu tulikuwa tunapiga dawa zingine zinaitwa junkie na ukipiga unalewa siku tatu. 

Katika picha za kitambo, Chris anaonekana bila meno na alipoulizwa sababu ya hilo alisema kuwa meno yalimwagika baada ya kugongwa na gari.

Alidai kuwa aligongwa na gari maeneo ya Jogoo road akiwa katika pilka pilka za kutekeleza wizi.

Nakumbuka tulikuwa katika korti ya Makadara baada ya rafiki yangu kukamatwa. Katika ile hali kuna mama alikuwa amebeba fedha nyingi za kulipa bondi lakini ilimbidi alipie korti kuu.

Alipotoka kwenda korti kuu nasi tukakimbia kumtegea kule ili tumuibie, na katika ile hali niligongwa na gari na nikang'oka meno ila sikuvunjika kokote. Pale Jogoo road nimegongwa na gari mara tatu.

Kwa hivyo pia nilikuwa mwizi ili niweze kujikimu mahitaji yangu ya madawa.