Ilikuaje: Pastor Susan aweka wazi kuwa 'Twa twa! hudumisha ndoa

pastor.susan.twa.twa
pastor.susan.twa.twa
Twa...twa.... twaa!  Ni kauli isiyo geni ambayo imesambaa kote mtandaoni na kutamkwa na wengi.

Kwenye awamu ya Ilikuaje na Massawe Japanni, Pastor Susan ameeleza kuhusu chimbuko la neno na maana yake kwa undani.

Yeye hufahamika sana kama Pastor Twa..! Twa..!, Susan mwenye umri wa arobaini hivi na mumewe Munene, anasema walikutana na mumewe wakiwa wadogo kanisani. Mapenzi yao yalianza wakiwa wadogo na alitamani sana kuolewa na kasisi.

Alipoulizwa kuhusu chimbuko la hili neno Twa twa, Susana alisema,"Awali tulizungumzia kwenye kanisa la wanandoa pekee kuhusu twa twa, hakukuwa na watoto,''

Familia hiyo ambayo kwa sasa wana miaka 20 ya ndoa na watoto watatu, wanasema ndoa yao imejengwa kwenye mapenzi na neno la Mungu.

"Kile kinacholeta ladha kwenye ndoa si pesa au chakula bali ni twa twa". Hilo neno twa, anasema wanatumia na mumewe kwenye ndoa yao kuhusu mapenzi.

Susan anasema kwamba wengi huficha, husema wanaumwa na kichwa, na huogopa kuweka bayana 'kuwa wanataka ku ...twa..twa.'

"Mimi na mume wangu hatuigizi kwenye twa twa, iwapo hatutatoshelezana, basi tunazungumza wazi wazi." alisema Susan.

Mbali na neno la Mungu, Susan na Mumewe wameiweka mbele masuala ya mapenzi kwenye ndoa.

Massawe alipouliza matatizo yao ya ndoa, alisema ni lazima kuwa na hayo. "Kuna mambo hutokea. "

Hata hivyo anasema kwamba dawa kamili ya ndoa ni mapenzi matamu, "Hata tukikosana na mumewe wangu kuhusu pesa, lazima tuwe na twa twa, kwa sababu hatujakoseana kwa sababu ya hiyo.

Kulingana na Susan, ndoa huvunjika kati ya miaka 6-7 na baaada ya hapo hali huwa shwari.

Aidha anasema kwamba makongamano ndiyo hujenga ndoa yao. Susan asema kwamba siri ni lishe bora.

"Hata kama siko, nahakikisha kwamba mume wangu amekula vizuri ili apate nguvu sawasawa," alisema.

"Chakula cha mume wako kiwe kizuri, kiwe cha asili, na isiyo na chumvi nyingi,"alisema Susan.