Ilikuaje: Size 8reborn aeleza jinsi mimba yake iliweza kutoka

Linet Munyali almaarufu Size 8 Reborn ni mwanamziki ambaye anafahamika sana katika sekta ya usanii, licha ya kuwa mwanamziki pia ni mke wa mume mmoja na mama wa mtoto mmoja.

Size8reborn ni mke wa Samwel Muraya anaye fahamika kama Dj Mo. na mwanamziki huyo ni kitinda mimba katika familia ya watoto sita.

Alipookoka aliweza kupitia changamoto ntyingi sana kwa maana mashabiki na wananchi walikuwa wameshaweka katika akili zao kuwa hajaokoka.

Katika safari yake ya wokofu amepitia changamoto kadhaa huku changamoto hizo zikimsababisha kukaa akiwa amejifungia kwa nyumba kwa wiki mbili.

Katika siku kadhaa zimepita, watu waliweza kusema kupitia mtandao wa kijamii kuwa mume wa mwanamziki huyo aliweza fanya mapenzi nje ya ndoa. Size8reborn alijibu nakusema..

"Huo si ukweli kuwa mume wangu alikuwa nje ya ndoa bali ni fununu tu za watu," Alisema Size8reborn.

Alisema kuwa mwanamke yeyote kutopata mtoto si kupenda kwake na watu wasidhubutu ataaa kuwaita majina mbaya hayafai kwa maana si kutaka kwake kutopata mtoto.