Ilikuaje: Tom Osanjo asimulia jinsi alivyopambana na depression

Mwanahabari mkongwe, Tom Osanjo ndiye aliyekuwa mgeni wetu leo katika kitengo cha Ilikuaje naye Massawe Japanni.

Osanjo alikuwa na shida ya kusombwa na mawazo (Depression) kwa miaka miwili, shida iliyomfanya kukimbilia pombe na dawa za kulevya ili kutuliza mawazo.

Mwanahabari huyo wa Nation alisimulia jinsi siku moja alivyoshuku kuwa ana depression na alipoenda kumuona mkuu wake kazini, alimshauri kwenda kumuona daktari wa akili ili a,weze kupata tiba.

Aliyenisaidia ni mkubwa wangu kazini. Nilianza ku suspect ni depression na nikasoma nikathibitisha nilipoenda kazini kuna counselor na tulipoongea akanituma kwa psychiatrist. Alieleza Osanjo.

Hii hali ya depression watu huichukulia vibaya eti umerogwa au wewe ni mwenda wazimu na kama unaweza ni vizuri kwenda kwa counselor.

Hata hivyo, alipoenda hospitalini, Osanjo hakuwa tu na shida ya kusombwa na akili ila tayari alikuwa ameathirika na pombe.

Waliniweka rehab kwani nilikuwa na depression na alcohol addiction kisha kuna madawa nilikuwa nimepewa na sikuwa nakunywa vizuri, dawa za anti depressants.

Rehab nilikaa kwa miezi mitatu na counselor na unapewa madawa na mle ndani kulikuwa na watu wa aina yoyote.

Je yeye hupambana aje na hali ile na mtu anapaswa kumchukulia vipi yeyote aliye katika hali ile?

Ukiwa na mtu kama yule usimpigie kelele kwani depression hufanya uhisi haufai. 

Nilipoweka story yangu kwa gazeti watu wamenipigia simu na nikaanza mpango wa kuelekeza watu kwa wenye watakaowasaidia.

Sasa hivi Osanjo ameanzisha huduma za kuwasaidia walio katika hali aliyokuwa nayo ili waweze kupata msaada na tiba wanayofaa.