Ilikuaje: Zena afunguka mwanzo mwisho kuhusu kimo chake cha maajabu

Binti huyu alikuwa na uzito wa kilo 122 na kusema kuwa kazi yake ni ya upishi na maishani mwake hajawahi kuwa na mwili mdogo.

https://www.instagram.com/p/B3rLX9TAjaC/

Hata hivyo, binti Zena alisema kuwa maisha yalikuwa magumu sana kwani alikuwa anshindwa kupumua na ata wakati wa kulala alikuwa anapata taabu sana.

Amini usiamini, ilimbidi binti huyu anunue kidude cha kumsaidia kupumua ambacho kilimgharimu pesa nyingi sana.

Vilevile, binti huyu alijaribu njia zote ili kupunguza kilo lakini hakuna kitu chochote kilichokuwa kikitendeka kisa na maana alikuwa na uzito ambao uliletwa na kutokuwa na usawa wa homoni.

Akizungumzia familia yake ilivyokuwa ikibabaika, alisema kuwa, mume wake alikuwa anampenda bado na hata  wanawe walimuelewa.

''Mume wangu alikuwa ananielewa na hata baada ya kuwaeleza watoto wangu ni nini kilichokuwa kikiendelea walinielewa.''

Hivyo basi, Zena aliamua kufanya upasuaji wa kupunguza kilo na akaweza kupunguza kilo 24 kwa muda wa miezi minne.

Binti huyu alisafiri mpaka nchini india kufanyiwa upasuaji na baadaye ilimbidi ale chakula kwa kiasi kidogo sana na sasa ako sawa anajipenda alivyo.

Licha ya hayo, alisema kuwa anawaomba watu walio na uzito mkubwa wajipende na wasijidharau.

Vilevile aliwaambia watu walio na uzito mkubwa wasiogope kutoka nje na kuzungumzia uzito wao kwani kila kitu kina suluhisho.

Ama kwa hakika,penye nia pana njia.