IMG_0013

”Nilikuwa nalala na wanaume watano.”Binti asimulia kazi ya ukahaba

Wahenga walisema penye nia pana njia na si uongo kwani binti aliyekuwa kahaba amefunguka wazi na kusema vile ambavyo alikuwa anafanya kazi ya ukahaba  na akaweza kuacha tabia ile.

Mzozo wa Mali waibuka baina ya Wajane Wanne wa Jacob Juma

Sadiki usisadiki,Sylvia alisema kuwa, akianza biashara hii alikuwa analala na wanaume watano au sita kila siku.

Binti huyu alianza biashara hii akiwa na umri wa miaka 15.

”Nilikuwa nalala na wanaume watano ama sita kila siku kwa sababu nilikuwa najua hii ni doo naingiza.Nilikuwa naingiza kitu 15k kila siku.”Sylvia alisema.

Vilevile,alisema kuwa hata yeye kuacha kazi hii,hakuacha kazi hii ghafla tu,alianza kushiriki ngono na watu watatu au wawili na polepole akaweza kuacha kazi hii.

Patanisho:”Hii ndio siku ya mwisho nakuongelesha.”Bwana amuambia mke wake

Aidha,kilichomfanya aingie kwenye biashara hii ya ukahaba ni maisha magumu.

Mama yake alifariki na ikabidi aishi na shangazi yake na kisha baadae mjomba wake akampeleka kwenye danguro.

Kwenye danguro,alianza kufanya kazi ya ukahaba na baada ya miezi mitatu akatoka.

Hata hivyo,baada ya miezi hiyo, alitoka huko na baada ya kufanya kazi kwenye hoteli alianza kazi hii ya ukahaba.

Siku yake ya kwanza kuanza kazi hii, ilikuwa ngumu sana kwani hakuwa anataka lakini pia alikuwa anatamani apate pesa ili arudi shuleni.

Baada ya miaka mitatu,binti huyu aliona kuwa kazi hii haina manufaa hata kidogo na akaamua kuacha.

Kidosho  huyu jina lake Sylvia alisema kuwa kwa sasa, kazi yake huwa kuwaongelesha kina dada wachanga waliojiunga na kazi hii ya ukahaba.

”Mimi nilikuwa nashangaa hawa watoto wadogo wanafanya nini hapa kwa sababu najua hawajui haki zako.”Sylvia alisema.

Sababu ya kumfanya aanze kazi hii  ya kuwaongoza kina dada wanaofanya kazi hii ni kwa sababu alikuwa anaona kuwa hata mabinti wachanga walikuwa wamejiingiza kwenye shughuli hii pasi nao kujua haki zao.

Mwisho kabisa,Sylvia alisema kuwa yeye hawezi waambia wasichana walio kwenye bishara hii waache ukahaba kwani hana uwezo wa kuwakimu maishani.

”Mimi siwezi waambia waache hii kazi kwa sababu sina kitu ya kuwapea kama kazi.Kitu naweza wasaidia nayo ni kuwaambia haki zao na kuwapa mawaidha watumie mbinu za kuwasaidia wasipate magonjwa ya zinaa.”Sylvia alisema.

Photo Credits: Amon Maghanga

Read More:

Comments

comments