Ilikuaje:hatujajaliwa kupata mtoto na mume wangu wa sasa-Nyota Ndogo

Leo katika kitengo cha ilikuaje tulikuwa na msanii wa nyimbo za bongo Nyota Ndogo almaarufu mwanaisha Abdalla na kutueleza jinsi alikuwa baada ya kunyamaza sana kama hajatoa muziki wowote.

"Niliachana na mume wangu wa kwanza mtoto wangu wangu akiwa na miaka minne na sasa yuko na miaka kumi na sita

Mume wangu wa pili uwa ananipa ruhusa ili mtoto wangu mbarack amuone baba yake mzazi, pia mume wangu, na kwa hakika si yeye alifanya niachane na mume wangu wa kwanza

Kwa hakika najuta sana kuenda katika mitandao ya kijamii na kusema kuwa ndoa yangu imevunjika

Hatujajaliwa na mtoto nikiwa na mume wangu

Ni mimi nataka watoto na mume wangu, si kwa sababu ya tamaa wala kutaka mali yake, tukienda  hospitali uwa tunaambiwa tuko sawa

Mama yangu alifanywa apinge ndoa yangu na mume wangu lakini sasa tuko sawa, uwa tunatembeleana naenda nchini Denmark miezi mitatu naye anakuja nchini Kenya miezi mitatu." Alieleza Nyota.

Nyota alisema alipumzika katika kutoa vibao kwa sababu ya ndoa yake.

"Nilipumzika kwa sababu hakuna vile ningetoa nyimbo zangu na kisha na safiri kila mara." Aliongea Nyota.

Kwa maoni yake Nyota alisema kuwa angependa kuongeaza watoto wawili na mume wake, msanii Nyota kuna wakati alialikwa kuenda kutumbuiza watu nchini USA.

Nyota alisema kuwa mapenzi ya ng'ambo ni ya kudekezwa lakini afrika si rahisi kudekezwa na mpenzi wako.

Hapo ndipo alipopatana na mume wake, kwa mengi zaidi tembelea mtandao wa kijamii wa Youtube. na kwa wimbo wake mpya tazama kwenye youtube