IlikuajeTulilawitiwa na watu wa karibu ,wasema john omondi na Henry Karanja wasimulia masaibu yao

IMG_0700
IMG_0700
aKatika kipindi cha ilikuaje John Omondi na Henry Karanja walitenga muda wao na kutueleza jinsi walivyo lawitiwa na watu wa karibu sana na wao.

John alianza  kusimulia masaibu ambayo alipitia mikononi mwa rafiki zake,

"Si kufahamu kama walikuwa mashoga ata rafiki yangu, waliniwekea dawa katika kinywaji changu ili nisijisikie walipokuwa wakifanya kitendo hicho

Walioninajisi walikuwa watano, wazazi wangu walijua niko shuleni nikisoma  kwa maana nilikuwa katika chuo kikuu

Sikuelewa walikuwa mashoga kwa maana nilikuwa nimesomea mashambani, nilipokuwa nafanyiwa kitendo hicho nilikuwa na miaka,21,

Baada ya kufanya hivyo walitoroka na kuniacha chumbani nikiwa pekee, nilijisikia kesho yake ambapo niliona nikiwa navunja damu sana

Niliamka lakini sikuwa na nguvu hata kindogo, nilizirai tena, niliamka hapo ndipo jirani yangu aliniona na akaenda kuita watu wakanipeleka hospitali."Alisimulia John.

John aliogopa kusema kitendo ambacho alifanyiwa  na hii hapa sababu yake

"Niliogopa kusema kwa maana niliogopa kukejeliwa na watu wa jamii, kama binadamu tunajua vizuri jinsi jamii ilivyo ukisema kitendo kama hicho ilhali umekuwa san." Alisema.

Mmoja wa amba walimlawiti alikuwa anaishi na yeye ni shoga, alipofikishwa hospitali hakuwafahamisha wazazi wake.

"Nilipoanza kuchumbiana niliambia mpenzi wangu kilicho nitendekea, nilipopona sikurudi shule kwa maana nilikuwa na haya nilianza kutumia dawa za kulevya kwa maana sikuwa najisikia mimi ni wa maana katika maisha

Niliambia wazazi wangu kilicho nitendekea baada ya kupona, kitendo hicho kiliniadhiri mpaka nilikuwa natumia pampers." Alieleza.

John hakutembea peke yake mbali alitembea na rafiki yake Henry Karanja ambaye alilawitiwa na mjomba wake na alikuwa na haya ya kusema.

"Nililawitiwa na mjomba wangu nikiwa na miaka ya,15, hapo nilikuwa kidato cha pili,hii baada ya mkutano wa kifamilia na mjomba wangu akambia baba yangu anataka tuende pamoja nyumbani mwake

Alikuwa na miaka,25, alipofanya kitendo hicho sikumwambia mtu yeyote, mbali nilijihisi nimekuwa shoga na nikaanza kutafuta mashoga wenzangu

Nilipata shoga wa Zanzibar, alinitumia nauli na nikakula alinipigia simu tena na kunitumia nauli tena, nilienda huko nikakaa kwa muda wa miezi mitatu huku tukifanya kitendo hicho

Baada ya muda niliokoka na nikaacha vitendo hivyo, nilikuwa nalipwa na shoga huyo pesa nyingi sana, nikiangalia nyuma ." Alisimulia Henry.

Kwa maelezo zaidi kuhusu walicho kipitia John Omondi na Henry Karanja tembelea Channel cha Youtube cha radiojambo.