'Ilikuwa ngumu kwako kujitokeza na kusema wewe sio mgonjwa?'Ujumbe wa Oscar Sudi kwa waziri Matiang'i

Mbunge wa Kapsaret Osar Sudi amemsuta waziri wa Mambo ya ndani Fred Matiang'i kwa kuwakamata jamaa ,2,waliochapsha habari feki kuwa ameambukizwa virusi vya corona na yuko (ICU).

Kupitia kwenye ukurasa wake wa facebook Sudi alisema kuwa Matiang'i angejitokeza na kusema kuwa si mgonjwa na kukataa madai hayo yaliosemwa na wawili hao.

Pia alisema kuwa amekuwa mwathirika wa habari feki kumuhusu, mara nyingi lakini hakuweza kulalamika wala kukana habari hizo.

Sudi alisema kuwa wawilo hao waliokamatwa, waliuwa wamekosa kazi, na kusema wanapaswa kuachiliwa haraka.

"Nataka kumuuliza Matiang'i unajulikana kama mtu mwema kwa wanahabari, unajua kujionyesha kwenye kamera ilikuwa ngumu kwako kujitokeza na kusema wewe sio mgonjwa?

Kwanini uwakamate Isaac Kibet na mlemavu Emanuel Kimutai? wengi wetu tumepitia jahanamu ikiwa ni habari feki,wewe ni mjinga, wawili hao walikuwa wanajaribu kupata riziki kwa mazingira ambayo wewe na wenzako mmeyafanya kutokuwa na kazi

Ni wanarika ambao hawana hatia na hawana kazi, waachilie vijana hao kwa haraka,hii nchi si yako." Sudi Alizungumza.

Haya yanajiri saa chachee baada ya makachero wa uchunguzi wa jinai(DCI) kusema wamewakamata wawili hao kwa kitendo hicho.