Ilikuwaje?: Tracy Wanjiru aelezea alivyonusurika kifo katika shambulizi la Westgate na DusitD2

Baada ya shambulizi la westgate kumaliza miaka mitano, magaidi wa Alshaabab hawakulaza damu bali waliweza kuwa na mipango ambayo watashambulia tena maduka ya ununuzi yanayokuwa na maelfu ya watu.

Westgate ilishambuliwa 21 Septemba 2013 ambapo zaidi ya watu hamsini walipoteza maisha na wengine kupata majeraha mabaya siku hiyo.

Katika shambulio hilo, Tracy Wanjiru almaarufu (Shiro) alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa ndani ya duka hilo magaidi walipo shambulia.

"Nilipokuwa hapo ndani niliona kifo kimefika hivo basi nilianza kumfikiria mtoto wangu nani atatimiza mahitaji yake nani atamchunga atakapokuwa akitoka shule"Aliongezea Tracy.

Kilichomfanya Tracy kusikia vibaya ni vile watu walikuwa wakiongea au kuzungumza mambo mabaya kumuhusu, imepita wiki moja lakini Tracy Wanjiru bado yupo kwenye mshtuko kwa yale yalitokea DusitD2 na ambayo alipitia.

Polisi walipowasili kuwaokoa kutoka mikononi mwa magaidi, hawakuamini kuwa kweli walikuwa ni polisi.Walidhani ni magaidi walikuwa wanawachezea.

Baadaye waliweza kuokolewa na kutolewa katika maeneo hayo.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be