‘Im tired, Nataka kusema ukweli sasa’ Mwanamke aliyezaa watoto 5 na makaka wa nyumba moja asema

Lady (3)
Lady (3)
Celia Githua amekuwa na siri kubwa  ambayo ameijua yeye pekee na watu wawili au watatu katika maisha yake , lakini sasa imekuwa nzito na anataka kupasua mbarika. Je , ndoa yake itaponea baada ya  ufichuzi huu ?

Celia aliolewa miaka 14 iliyopita na mume wake alikuwa akifanya kazi nchini Ujerumani. Baada ya kuishi naye kwa mwaka mmoja aliamua kurejea Kenya ili kujenga katika shamba lao walilonunua na kuanza kuzoea maisha ya ‘nyumbani'. Akiwa Ujerumani aliweza kupata mimba ya mtoto wake wa kwanza lakini kilichofuatia ni kirefu na kisa chake ni kama filamu ya Nigeria .

Kwa ufupi, katika nyakati tofauti muda huo wote Celia amekuwa akipata mimba kwa kushiriki  mapenzi na ndugu za mume wake wane ambao wanaishi Kenya. Watoto wake wote watano ni kila mmoja wa kaka hao na kwa sababu wanafanana wote, wengi wanajua kwamba watoto wote ni wa mume wake Mark anayeishi Bonn, Germany. Kuhusu jinsi alivyofika hapo,Celia anasema kwamba alikuwa tu na wazo la kufanya hivyo na mwanzoni ilikuwa kama mzaha na pia alitaka kujua tu itakuwa vipi iwapo mwanamke mmoja anaweza kupata mtoto wa  kaka za mume wake. Anasema ;

“I was just Curious! Sikujua  nitafika hii stage ya kupata mtoto na kila mmoja wao but at the end  of the day ,imefanyika’.

Celia  sasa  anasema kwamba  imeanza kuwa vigumu kwake kuficha siri hii kwa sababu kaka wawili  wamejua kwamba  alizaa watoto nao na sasa wanalitumia hilo kama chambo cha kumpunja pesa ili wasimuambie mume wake.

Anasema amelazimika kuanza kufikiria kuhusu njia ya kumfichulia mume wake kwamba watoto wane kati ya watoto wao 5  ni wa kaka zake. Huenda ndoa yake itavunjika baada ya ufichuzi huo lakini Celia anasema kinachompa  motisha ya kuwa mkweli ni kwamba watoto hao wote ni damu moja na endapo atafukuzwa na mume wake, basi kila kaka atalazimika kumchukua mwanawe na kuanza kumwajibikia .

‘Siigopi kwa sababu najua  by now ukweli kijotokeza, kila kaka atalazimika kumchukua mtoto wake na amtunze. Mimi niko tayari kuwajibikia makosa yangu.’ Celia anasema

Celia anasema  yote yalianza wakati alipomaliza kujenga nyumba yake, kisha shemeji zake wakaanza kuja kumtembelea na kwa sababu mume wake alikuwa mbali anasema alikuwa na hisia na akajipata akiwashawishi walale huko kwa siku moja au mbili. Baada ya mmoja kuja, wengine bila kujua pia wangekuja kumtembelea pale bomani nyakati tofauti. Mume wake pia akiwa likizoni alikuwa anarejea Kenya na ndiposa anaamini kwamba watoto wale wote ni wake lakini Celia anafahamu ukweli .

Sio siri kwamba kuna wanawake walio na watoto na wanaume mbalimbali lakini hii ya Celia ya kuwa na watoto na kaka wa nyumba moja ni historia ya kipekee au rekodi ya siri ambayo hata walioivunja hawawezi kujitokeza kusema ukweli .