Inakuaje mkewe Ken Okoth ni mfuasi sugu wa MacDonald Mariga?

Ann_Thumbi_with_her_Jubilee_counterparts__1568271714_55186
Ann_Thumbi_with_her_Jubilee_counterparts__1568271714_55186
Kifo  cha aliyekuwa mbunge wa Kibra Ken Okoth kiliibua maswala mengi ambayo hayakuwa yanajulikana.

Kulikuwepo na siri kubwa maishani wa mwanasiasa huyu ambayo watu wengi hawangeweza kufahamu.

Soma hadithi nyingine:

Kikubwa kilichovuja ni kwamba sio tu kwamba alikuwa katika mahusiano ya kimapenzi na Ann Thumbi bali ata walifanikiwa kupata mtoto pamoja.

Vipimo vya msimbojeni vilidhibitisha kwamba ni kweli walikuwa na mtoto.

Kulikuwa na hali ya sintofahamu kuhusu mtoto huyu.

Sasa mambo yanaonekana kuchukua mkondo tofauti wakati Ann Thumbi alipowasili katika ofisi za tume ya IEBC huku akiandamana na Mariga.

Inakuaje anaunga mkono Mariga wala sio Imran?

Soma hadithi nyingine:

Kama kweli ana uhuru wa kufanya uamuzi wa kiongozi atakayemchagua.

Ila ikija katika maswala ya familia labda kuna baadhi ya vitu labda hawaendi sawa na anachokifanya ni njia moja ya kuwakomoa wanafamilia.

Swala hili lilizua mjadala katika mitandao ya kijamii wengi wakiona kwamba sio tatizo akitangaza kumuunga mkono Imran.

Katika mahojiano na vyombo vya habari, Ann alisema,

Soma hadithi nyingine:

"Niliteuliwa katika bunge la kaunti ya Nairobi chini ya mwavuli wa chama cha Jubilee. Kwa hivyo nina jukumu kubwa kufuata uamuzi wa chama kuhusu uteuzi wa mgombeaji Kibra. Uamuzi wa Jubilee ni Mariga na natakiwa nimuunge mkono."