Inaudhi sana!' Wimbo mpya wa Alikiba Dodo wapungua views hadi 700

NA NICKSON TOSI
Masaa tu baada ya msanii kutokea Bongo Alikiba kutoa wimbo wake mpya wa Dodo na kuuweka katika mitandao yote ya kijamii, imebainika wazi kuwa wapinzani wake walitapeli [hacking] idadi ya watu waliokuwa wameutazama wimbo huo kwenye mtandao wa Youtube na kurudisha idadi hiyo kuwa ya chini mno hadi watu alfu 700.
Hamisa Mobetto ambaye ameshirikishwa kwenye video hiyo alighadhabishwa na swala hilo na kuandika hivi.

Ukuaji kimuziki katika taifa la Tanzania huwa na changamoto zake. Wakati mtu anapofanya wimbo wake na kutumia muda wake, pesa na kila kitu, lazima kuna watu watalemaza kazi yake. Aliandika hamisa

‘Kazi nzuri ni kazi nzuri tu. Embe halidondoki kutoka kwa mti lenyewe, lazima mtu aukwee na hatimaye kulichuma. Aliongeza Hamisa.

Licha ya kitendo hicho kujiri, wafuasi wa Alikiba wameendelea kuutazama wimbo huo kwenye kitandazi cha Youtube na sasa umerejea na watazamaji milioni 1.
 Tazama wimbo wenyewe uu hapa