'Inauma sana kuwa wanangu 3, wana ujauzito-CS Magoha awaonya wazazi

Waziri wa elimu George Magoha ameeleza masikitiko yake kwa wazazi wa wanafunzi watatu wa kidato cha kwanza ambao alisisitiza kusajiliwa na kupewa nambari ya usajili ya shule ya upili.

Huku akiwaita wana wake Magoha, alieleza kwa ajili ya muda mrefu ambao wanafunzi wamekaa nyumbani kwa ajili ya virusi vya corona wazazi wa watoto hao watatu hawakuweza kuwalinda iwezekanavyo.

Na kwa ajili ya uzembe wao wanafunzi hao sasa wana ujauzito kila mmoja.

"Kwa habari za kusikitisha wizara hii imejuwa kuwa wazazi wengi hawalindi watoto wao vyema wakati huu wako nyumbani kwa ajili ya janga la corona

Kwa mfano inauma sana baada ya mimi mwenyewe kwenda katika makazi duni na kuwachukua wasichana na kisha kusisitiza wapewe usajili katika shule za upili 

Na kuwalipia karo na hata kuwalipia baadhi yao karo ya shule ya miaka minne sasa wana ujauzito kwa muda mfupi ambao wamekuwa nyumbani." Alieleza Maghoha.

Aliwauliza wazazi kuzaa watoto ambao wanaweza kuwaangalia na kisha kuwaonyesha upendo wao wakati wamekaa nao nyumbani.

"We should only produce those children we are able to take care of. If you don't have the time to look after a child then perhaps you have no business producing children.

"I want to state without fear of contradiction that parents have to change their mindsets and love their children by spending time with them...I think that is what is lacking and I hope this won't to any of my many other daughters who are at risk especially in the slums but even in other homes where parents have a carefree attitude." Alizungumza Maghoha.

Magoha aliwasihi wazazi pia kuangalia chochote watoto wao wanatazama kwenye mitandao ya kijamii ili wasipate mambo ambayo hayastahili, kwa maana wawindaji wamo mitandaoni wakiwa tayari kuwapotosha wanafunzi wengi.