848af1d06b3baaed

Inspekta Mwala achamba magazeti kuu nchini. Asema yeye sio muuaji

Mcheshi wa vipindi vya runinga Inspekta Mwala hajafurahia jinsi magazeti kuu nchini yalivyoshobokea tukio la ajali Kaloleni. Akijawa na ghadhabu kubwa, Mwala amekashifu jinsi habari hizi zinasambaa kama moto jangwani badala yake kumakinika katika kuchapisha habari muhimu. Kulingana na mcheshi huyu, magazeti yanafaa yazingatia zaidi njaa na ukame uliopo maeneo mbalimbali nchini.

Katika chapisho mtandao wa Twitter, Mwala anateta kuwa yeye sio muuaji. Asema kuwa angelikua muuaji basi angejiunga na kundi la wanamgambo la Alshabaab.

Soma mengine:

Ni gumzo mtaani. Mithika Linturi na Kitany wana majumba ya kifahari kweli

“Nasikitika kwa kile kilichofanyika. Nasema pole kwa familia. Ningelikuwa muuaji basi ningejiunga na Alshabaab.” Asema Mwala.

Mkuu wa polisi kaunti ya Kilifi Patrick Okeri amesema kuwa Mwala alikuwa ameendesha gari aina ya Toyota Axio usiku wa jumatatu alipotatizika barabarani na kumgonga Samuel Mwaki.

Soma hapa:

Marianne Kitany afunguka A-Z jinsi simu ya Mithika Linturi ilisheheni picha za ngono

Muigizaji huyu alizuliwa kwa muda katika kituo cha Polisi cha Rabai baadaye kuachiliwa kwa dhamana ya kitita cha pesa.

“Tulimwachilia kwa sababu familia ilichukua muda mrefu kuandikisha ripoti katika kituo cha polisi. Tunasubiri kuona iwapo kutakuwa na makubaliano na familia ya mwendazake kabla tuchukue hatua,” alisema Okeri

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments