.Amesema haifai kwa wakenya kuendelea kupitia mahaingaiko kabla ya kupata stakabdhi hizo .“ Tunatangamana na wananchi wetu kila siku hasa wakiwa wanyonge na mateso nilioona wakipitia mwaka jana sio jambo linalofaa kukubalika’ .Amesema waziri huyo.
“ Hatuwezi kuchukuliwa kama watoaji wa suluhisho ilhali wakati huo huo tunakuwa chanzo cha machungu . Hili lazima likome!’ amefoka Matiang’I . Waziri huyo amemwagiza katibu wa kudumu anayeshughkilia huduma za wananchi kuhakikisha kwamba ahadi za utendakazi na uadilifu wa idara za serikali zinatekelezwa . Pia amewaagiza makamishna wa kaunti kufanya ukaguzi wa kushtukiza katika vituo vya kutoa huduma za serikali na kuripoti hatua zinazofaa kuchukuliwa kuboresha utendakazi na utoaji wa huduma kwa wnaanchi .