Itakulazimu kufanyiwa vipimo vya Corona kabla ya kulazwa katika kituo cha afya - Wizara ya Afya yasema.

Kama njia ya kukabiliana na kuenea kwa virusi vya corona nchini, serikali inasema iwapo kuna mkenya atakayelazwa katika hospitali za humu nchini, ni sharti afanyiwe vipimo vya kubaini iwapo ana virusi vya Corona.

Serikali pia inapania kuanza kuwapima wagonjwa wote waliolazwa katika hospitali za humu nchini ili kubaini iwapo wameambukizwa virusi hivyo.

Mkurugenzi mkuu wa afya katika wizara ya afya nchini Patrick Amoth amesema hatua hiyo pia inapania kuwakinga wahudumu wa afya katika hospitali hizo na pia kuwakinga wafanyakazi wengine wanaohuduma katika hospitali mbalimbali  nchini .

“It is likely that when an asymptomatic case is admitted to hospital, they may spread the virus to the healthcare workers or other patients in the ward, we need to be able to protect those people,” amesemaDr Amoth

Amoth ameongeza kuwa serikali itaanza kusambaza vifaa vya kuwapima wakenya kuhusiana na virusi hivyo ili kufanikisha ajenda yake ya kutaka kujua ni idadi ngapi ya watu walioathirika nchini.

‘These test-kits will be distributed in a stepwise manner to ensure that this requirement will not be used as a basis of denying Kenyans treatment for other conditions,” aliongezea Amoth