Its Official! Mpenzi wa zamani wa Harmonize Wolper achukuliwa na Young Killer

Uvumi umekuwa ukizagaa kuhusu kuwepo kwa uhusiano wa kimapenzi  kimapenzi kati ya rapa Young Killer na staa wa filamu Jacqueline Wolper na sasa ithibati imepatikana kwamba huenda pana ukweli katika uvumi huo  kwa sababu   wawili hao wamethibitisha hilo katika mitandao ya kijamii.

Wakati wa maadhimisho ya siku ya siku ya wanawake duniani siku ya jumapili tarehe nane  Young Killer alitumia fursa hiyo kupost picha yake akiwa pamoja na Wolper katika mtandao wa kijamii wa Instagram na kuandika.

"Yaani wewe mwanamke usiku silali, mchana Tarime, kheri ya siku ya wanawake duniani".

Baada ya muda mfupi kupost picha hiyo naye Jacqueline Wolper akaja ku-comment kwa kuandika ;

"Ahsante sana Erick kwa kunipenda mimi, nakupenda pia ngosha".

Kwa sababu ya maelezo na picha hizo basi ni rasmi kwamba Wolper ameamua kuchukua hatua nyingine kusonga mbele baada ya kuachana na mwanamuziki Harmonize .