Iwapo hutaki kuwafunza watoto basi acha:Magoha awakashifu wanaopinga masomo ya ‘kijamii’

mAGOHA
mAGOHA
Waziri wa elimu George Magoha amewashauri wasiotaka kuwafunza watoto katika mpango wa kutoa mafunzo  ya kijamii majumbani kuacha

Magoha  alikuwa kizungumza kuhusu pingamizi dhidi ya mpango wa kutumia mfumo wa nyumba kumi kuendelea kuwasomesha watoto nyumbani wakati huu wa janga la corona baada ya shule kufungwa kama njia ya kuzuia usambaaji wa virusi vya corona .

" Kugeuka na kuanza kubadilisha mambo kuhusu mpango huo ni jambo la kusikitisha .mpango huu ulifaa kuhakikisha kwamba watoto wanasomeshwa katika maeneo walioko’ amesema Magoha

Akizungumza huko Eldoret  Magoha amesema kuna habari za kupotsha zinazoenezwa kuhusu mpango huo .

" Naskia mambo mengi kuhusu mpango huu… iwapo unaishia katika eneo  lililozizngirwa na kuna watoto 30 , na mwalimu mmoja huo ,unahitaji  PPE’s za nini ?’

" kama hutaki kuwafunza watoto wacha ..Usijisumbue! watoto ni wenu . Ni rahisi kwa njia hiyo

Akisema kwamba serikali haina mpango wa kuzifungua shule Magoha alisema wakenya wanafaa kukomesha dhana kwamba ni serikali ndio iliyoleta virusi vya corona .

" Hatutafungua shule .masomo ya kijamii  sio mpango wa kufungua shule’

" watu wanafikiria kwenda shule ni kuhusu kalamu na karatsi .kuna vitu vingi vya kuwafunza watoto’ alisema