Liwe funzo! Wachina walionaswa kwa video wakimcharaza mkenya warudishwe makwao

wachina
wachina
Wachina wanne waliotiwa mbaroni baada ya mmoja wao kurekodiwa akimcharaza mkenya mmoja, wamefukuzwa nchini na kurudishwa kwao nyumbani.

Wanne hao waliondoka katika uwanja wa kimataifa wa JKIA saa mbili usiku wakielekewa Uchina jana.

Hii ni kwa mujibu wa agizo la mahakama kuu ya Milimani iliyoamrisha wanne hao wanaojulikana kama Deng Hailan, Chang Yufall, Ou Qiang na Yu Ling.

Maafisa kutoka kitengo cha DCI huko Kilimani ambao walikuwa wamezuia wachina hao waliwakabidhi washukiwa hao wanne kwa maafisa wa idara ya uhamiaji.

Amri ya kuondolewa kwao hapo awali ilikuwa imesimamishwa na Mahakama kuu baada ya watuhumiwa hao wanne kuwasilisha maombi ya kupinga agizo hilo.