Jaji Mkuu Davidi Maraga akosa kwenye uzinduzi wa BBI, kunani ?

maraga
maraga
Jaji mkuu David Maraga hakuhudhuria hafla ya uzinduzi wa pendekezo la maridhiano la BBI Jumatano kwenye ukumbi wa Bomas of Kenya.

Awali Maraga alikuwa ametishia kutohudhuria baadhi ya makongamano ya serikali na kwa kweli amedhihirisha kuwa haikuwa vitisho tu.

Katika halfla ya Jumatatu, kulikuwa na wajumbe zaidi ya 4,700 wakiwemo viongozi wakuu serikalini.

Jaji Maraga alionyesha mafadhaiko yake na kudai kwamba ofisi yake haipewi hadhi inayofaa.

Hata hivyo, haikubainika wazi iwapo Maraga alikuwa amealikwa, kusahaulika au alisusia uzinduzi huo.

Mnamo Novemba 4, Maraga aliapa kutohudhuria baadhi ya mikutano ya serikali hadi afisi yake itakapopewa hadhi inayofaa.

"Hadi nitakapopewa hadhi inayofaa, nitachagua mikutano ya kuhudhuria," Maraga alisema.

"Jaji Mkuu hapewa hadhi kama ilivyo mawaziri na makatibu hupewa," alisema.