Jamaa Afariki Baada Ya Kubugia Pombe Ya Aina Ya Busaa, Siaya

busaa.000
busaa.000

Mwanaume mmoja kwa jina George Otieno mwenye umri wa miaka 40 amefariki baada ya kuanguka na kuzirai alipokuwa akitoka kwenye maeneo ya kuuzia pombe ya aina ya Busaa huko Rarieda kaunti ya Siaya.

Inadaiwa marehemu alikuwa shambani kabla ya kualikwa na rafikiye katika klabu hiyo ya busaa huku akiacha shughuli ya shamba kuenda kubugia pombe.

Akithibitisha kisa hicho chifu wa eneo hilo, Agola Ochola, alielezea kuwa marehemu alizirai karibu na boma lake huku juhudi za kumkimbiza hospitalini zikiambulia patupu na kufariki kabla ya kufika hospitalini.

Aliongezea kuwa tayari mwenye klabua hiyo na rafikiye wametiwa mbaroni ili kusaidia katika uchunguzi huku mwili wa marehemu ukihifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Madiany.