Jamaa akamatwa akikojoa kwenye jiwe la kumbukumbu ya polisi aliyeuawa

pVStFaJM.jfif
pVStFaJM.jfif
Mwanamume mmoja mwenye miaka 28, amekamatwa kwa madai ya kukojolea kibao cha kumbukumbu ya afisa wa polisi aliyeuawa wakati wa maandamano eneo la kati mwa mji wa London.

Kulingana na Polisi wa Metropolitan, jamaa huyo anazuiliwa Essex, kaskazini mwa London, baada ya kujisalimisha katika kituo cha polisi.

Marehemu Keith Palmer 48, alidungwa kisu akiwa kazini katika shambulizi la Westminster la Machi 22, 2017 na alikuwa miongoni wa watu watano waliouawa na Khalid Masood.

Jiwe la kumbukumbu lake liliwekwa eneo la Carriage Gates, Westminster, pale ambapo Palmer aliuawa.

Polisi walikabiliana na waandamanaji jijini London siku ya Jumamosi Juni 13, ambao walikuwa wanakashifu ubaguzi wa rangi nchini humo.

Waandamanaji kadhaa walikamatwa kwa makosa tofauti yakiwemo, kufanya vurugu, kushambulia polisi, umiliki wa silaha, kuvuruga amani, kuwa walevi na kusababisha vurugu pamoja na umiliki wa dawa za kulevya.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson alishtumu vurugu hiyo na kusema "Uhalifu unaofanywa kwa misingi ya ubaguzi hauna nafasi katika maeneo yetu." 

Polisi walivamiwa na waandamanaji ambao wengine walikuwa wanaharakati wa mrengo wa kulia baada ya maelfu yao waliokuwa wamekusanyika kusema kuwa wanalinda masanamu yasiharibiwe.

Maandamano yamekuwa akitokea kote duniani kufuatia kifo cha George Floyd ambaye alifariki mikononi mwa polisi nchini Marekani.

Mmarekani huyo mweusi alifariki kutokana na kukosa hewa baada ya polisi mwenye asili ya kizungu kumuekea goti shingoni wakati wa kukamatwa.