Jamaa Akamatwa Na Kilo Kumi Ya Bangi Ya Thamani Ya Shilingi Milioni Nne - Migori

Polisi huko Rongo kwenye kaunti ya Migori wamemkamata mtu mmoja anayedaiwa kupatikana na bangi ya kilo kumi ya thamani ya shilingi milioni nne katika kizuizi cha magari cha mji wa Rongo usiku wa kuamkia leo.

Kwa mujibu wa OCPD wa Rongo, Jonathana Kisaka Muganda, mwanamme huyo Morris Odhiambo mwenye umri wa makamu anadaiwa kupatikana akisafirisha bangi hiyo kwa gari aina ya probox lilillokuwa likielekea mjini Nairobi kupitia mjini Kisii ambako kuna soko la kuuza bangi hiyo.

Aliongeza kuwa mshukiwa huyo ambaye alikuwa pekee yake kwenye gari hilo amezuiliwa katika kituo cha polisi cha Kamagambo mjini Rongo akisubiri kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka dhidi yake.