Jamaa akanusha kumuua mpenziwe kwa ajili ya godoro

Mwanabiashara mmoja jana alishtakiwa katika mahakama moja Nairobi kwa kosa la kumuua mkewe walipokuwa wakipigania godoro na vyombo vya nyumba.

John Otieno alikana madai hayo mbele ya hakimu mkuu Merisa Opondo. Aliwachiliwa kwa dhamana ya shilingi Sh200,000.

Otieno anakabiliwa na shtaka la kumuua Eunice Adhiambo nje mwa nyumba ya kukodi ya bwanake mpya katika mtaa wa Soweto, Nairobi October 12.

Mahakama ilielezwa kuwa Otieno na Adhiambo walikuwa wameoana na pamoja wamejaliwa watoto watatu lakini walitengana baada ya wawili wa wanao kuaga dunia.

Adhiambo aliolewa tena na kuhama pamoja na mtoto wao mwenye umri wa miaka miwili.

Siku ya tukio hilo, Otieno alienda kwa nyumba ya mumewe Adhiambo, bwana Eric Oloo kudai mali aliyodai Adhiambo aliondoka nayo. Wawili hao hawakuelewana.

Majirani walienda kuingilia kati baada ya kusikia kelele nyumbani kwa Oloo na kumkuta Otieno akikusanya vitu vya nyumbani ambavyo alidai ni vyake.

Otieno alisisitiza kuwa godoro lililokuwa juu ya kitanda cha Oloo lilikuwa lake na akalidai. Lakini Adhiambo alisema alikuwa ameacha godoro lake kwenye dari ya nyumba yao ya zamani na likubali kwenda kuichukua.

Lakini jirani na mtunzaji wa Oloo aligundua kwamba Otieno alitaka kumtoa Adhiambo nje ya nyumba ili amdhuru. Walijitolea kuandamana nao wakati alipoenda kuchukua godoro lile.

Adhiambo alitoka huku akifuatiwa na Otieno lakini wakati yule jirani alirudi kuchukua koti lake huku yule mtunzaji akifunga nyumba yake ili awafuate, huo ndio wakati Otieno alimshika na kumvuta Adhiambo nje ya eneo la ghorofa, akampiga na kumuangusha chini kabla ya kumdunga paja.

Jirani huyo, ambaye ni shahidi mkuu wa upande wa mashtaka, aliona Otieno akitumia kisu kilichojaa damu kuwatisha wakazi ambao walijaribu kumzuia kukimbia.

Huku akivuja damu nyingi, Adhiambo aliachwa akiwa amelala chini. Otieno alitupa kisu hicho umbali wa mita 100 kabla ya kutoweka. Kisu hicho kimeorodheshwa kama maonyesho mahakamani.

Adhiambo alikimbizwa katika Hospitali ya Mama Lucy ambapo aliaga dunia.
Otieno alikamatwa katika chumba kimoja alichokodisha katika eneo la Masimba huko Kayole baada ya tukio hilo.
Kesi hiyo itaskizwa Machi 10 mwaka ujao.
-The Star