Jamaa aliyejihami kwa kisu ajaribu kuingia ikulu

Mwanafunzi mmoja wa chuo kikuu mwenye umri wa miaka 25 alipigwa risasi Jumatatu na polisi wanaoshika doria katika Ikulu alipojaribu kuinguia ndani kwa kuruka ua.

Brian Kibet Bera, mwanafunzi wa mwaka wa tano uhandisi wa mitambo katika chuo kikuu cha JKUAT awali alichapisha katika mtanadao wa Facebook kwamba atavamia ikulu.

Amelazwa katika hospitali kuu ya Kenyatta kwa sasa na analindwa na polisi baada ya kupigwa risasi ya bega.

Kibet alikua amejihami kwa kisu jana saa 4:15 jioni akijaribu kupanga ukuta karibu na 'Gate B', kwa mujibu wa ripoti ya polisi.

"Alichomoa kisu hali iliyopelekea polisi kumfyatulia risasi na kumjeruhi bega lake la kushoto," ripoti hio inasema.

Mkuu wa polisi wa Kilimani Michael Muchiri alisema kua mshukiwa huyo alipelekwa kwa kituo cha polisi cha Kileleshwa kabla ya kulazwa hospitalini.

Polisi wameanzisha uchunguzi kubaini madhumuni ya kitendo hicho.