Jamaa Aliyenyofoa Sehemu Za Siri Za Mpwa Wake Anusurika Kifo Baada Ya Kupewa Kichapo Cha Mbwa

Polisi huko Wundanyi kaunti ya Taita Taveta wamewatawanya wananchi waliojawa na ghabadhu na kumtia mbaroni mwanaume mwenye umri wa miaka 27 anayedaiwa kumkata sehemu nyeti binamu yake jana.

Akithibitsha kisa hicho kamanda wa polisi katika kaunti hiyo Fredrik Ochieng amesema mshukiwa anaendelea kupokea matibabu katika hospitali moja huko Wundanyi akisubiri kufikishwa mahakamani.
 
Mtoto huyo mwenye umri wa miaka tano alikatwa nyeti zake katika hali ya kuatatanisha na anapokea matibabu katika hospitali ya wanawake ya Nairobi.