Jamaa aliyewabaka wanawake 40 chini ya mwaka mmoja akamatwa na polisi

227bb8830bd57876
227bb8830bd57876
Polisi nchini Nigeria wamemkamata mwanamume mmoja anayedaiwa kuwabaka wanawake 40 chini ya mwaka mmoja. Jamaa huyo alikamatwa baada ya mwanamke mmoja mkaazi wa mji wa Dangora kaskazini mwa Nigeria kumpata akiwa amejificha katika chumba cha watoto cha kulala.

Kiongozi wa mji huo, Ahmadu Yau, alisema kukamatwa kwa mshukiwa huyo ni hatua kubwa ambayo wamepata katika kukabiliana na uhalifu huo.

"Watu wa Dangora wanafurahia sana hatua zilizochukuliwa na tunatumaini haki yao itatekelezwa,"alisema Yau.

Wakaazi wa Dangora walidokezea kwamba walikuwa wakiishi kwa woga mwaka 2019 na wengine hata kuchagua kusalia ndani ya nyumba zao kwa sababu wabakaji walikuwa wanaruka ua na kuingia majumbani kuwabaka wanawake.

Visa vya ubakaji na mauaji ya wanawake nchini Nigeria vimekuwa vikikithiri siku za hivi karibuni hali ambayo imewapelekea wananchi kumeza funda chungu la mate.

Kulingana na dada yake marehemu, Judith Omozuwa, Uwavera alikuwa anajisomea vitabu vyake ndani ya kanisa la Redeemed Christian Church of God(RCCG), karibu na nyumbani kwao Benin City wakati wa tukio hilo.

Judith alifichua kwamba dada yake mpendwa alibakwa kabla ya kuuawa na wahalifu hao. Uwavera alikimbizwa hospitalini baada ya mlinzi kumpata sketi yake ikiwa imechanika na blauzi yake ikiwa imelowa damu.

Mwanafunzi huyo ambaye alikuwa na ndoto ya kuwa muuguzi, alikata roho hospitalini siku ya Jumamosi, Mei 30, kutokana na majeraha aliyopata baada ya kushambuliwa.

Wananchi walizua hamaki mitandaoni kufuatia mauaji hayo ya kinyama huku kampeni ya kutaka atendewe haki ikienea nchini humo.