Jamaa amchoma mkewe kwa kumpikia wali badala ya githeri

  Mwanamke mwenye umri wa miaka 27 anauguza majeraha katika  hospitali moja ya kibinafsi huko Mwea ,Kirinyaga baada ya kuchomwa na mumewe kwa kumpikia Githeri badala ya wali .

Kwa mujibu wa shangazi yake mwathiriwa , Peter Ngugi mwenye umri wa miaka 32  alihamakishwa na hatua hiyo na kumtupia mkewe stovu iliyokuwa ikiwaka .OCPD Lucas Chebet amesema mshukiwa  anasakwa ili kukamatwa na atafikishwa kortini . wawili hao wamekuwa katika ndoa kwa miaka miwili na wana watoto wawili .