Jamaa ampiga mkewe hewani akijaribu kupatanishwa

Naomi aliomba apatanishwe na bwana Polycarp ambaye alimpiga siku kadhaa zilizopita.

"Kwanza juzi alipea watoto fedha wakanyolewe lakini hawakunyolewa. Sasa badala aulize mbona hawakunyolewa aalianza kunipiga akidai kuwa niliwaambia nitawashuka lakini sikuwashuka." Alieleza Naomi.

Tena asubuhi nikamtuma mizigo kwani anafanya biashara tao lakini akaanza kunitusi na nikamuacha. Kuna sister yake tunaishi na yeye alikuja juzi, sasa akienda kazini nikamzindikisha nikarudi na akaanza kunigombanisha akiniuliza anafanya nini huku.

Nikamweleza yeye ndiye anafaa kumweleza kwani mimi kama shemeji yake ataona vibaya." Alisimulia Naomi akiongeza kuna vituko vingi vilitokea isitoshe hupigwa mara kwa mara.

Aliongeza kuwa walianza kubishana miaka mingi iliyopita kwani alikuwa na tabia ya kuleta wanawake wengine kwa nyumba bila aibu na akiuliza ana pigwa, na licha ya hayo yote aliendelea kuvumilia.

Baada ya kuangazia kesi yake, bwanake ambaye alikuwa nyumbani alimvamia akiwa anazungumza na watangazaji Gidi na Ghost hewani.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be