Jamaa amtembelea mpenzi wake na kumpata akifanya mapenzi na mwanamume mwingine,awadunga kisu wote

Mwanamme mmoja amemwua mwingine kwa kumdunga kisu  katika kituo cha kibiashara cha Eming huko Mogotio kaunti ya Baringo baada ya  kumpata kitandani na mpenzi wake .

Mshukiwa aliyetambuliwa kama  Abraham Kipsosion Kibor, anadaiwa kuondoka sehemu yake ya kazi saa kumi na moja jioni ili kumtembelea mpenzi wake katika nyumba ya kukosi bila kumpa notisi kwamba anakuja na alitamaushwa kufungua mlango na kupata akiwa na mwanamme mwingine  ambaye sasa ni marehemu   Michael Kipyegon mwenye umri wa miaka 36 .

Polisi katika kituo cha Eming waliothibitisha  mauaji hayo wamesema mshukiwa baadaye alijisalimisha kwa polisi  na pia alimdung kisu mpenzi wake baada ya kumuua  jama aliyekuwa akifanya mapenzi naye .

Polisi waliwakimbiza wawili hao katika hospitali moja huko Eldama Ravine  lakini mwanamme aliaga dunia  kwa ajili ya majeraha aliopata kifuani . mwanamke naye yupo katika hali nzuri baada ya kutibiwa . kisu kilichotumiwa kimehifadhiwa na polisi ili kutumiwa kama ushahidi huku uchunguzi ukianzishwa .