Jamaa amuua babake baada ya kugombania kipande cha ugali

Polisi wa shinyalu kaunti ya kakamega wanamsaka kijana wa miaka thelathini kwa madai ya kumuua babake wa miaka themanini kufuatia mzozo wa kipande cha ugali katika kijiji cha shiswa.

Wakazi wamesema kijana huyo Musa Luvowa amekua mtukutu na kuwashangaza wazazi pamoja na wakazi.

Kwingineko, Polisi mmoja wa AP cheo cha constable mjini Kakamega amemuua mwenzake kwa kumpiga risasi kufuatia ugomvi kuhusu mwanadada.

Kaimu ocpd wa kakamega Sammy Nyongesa amesema wawili hao walizozana kimzaha kabla ya mwenzake kumpiga risasi na kwa sasa amekamatwa.

Hayo yakijiri,

Afisa mkuu wa idara ya upelelezi katika kaunti ya vihiga joshua cheptoo amesema kuwa idara hiyo itazidi kushirikiana na idara ya mahakama kuhakikisha kuwa suala la uhalifu linakomeshwa katika kaunti hii.
Hii ni baada ya Mahakama ya hamisihapo jana kuwahukumu watu watatu wakiwemo wanaume wawili na mwanamke mmoja kwa makosa ya uhalifu ambapo walivitekeleza visa vya uhalifu katika maeneo mbalimbali yakiwemo Trans Nzoia, Eldoret na vihiga.
Hakimu wa mahakama hiyo Maureen Nabibya aliwahukumu watu hao josephat kiptoo na hillary lidolo miaka hamsini mtawalia na akamhukumu naomi wanjiru miaka kumi. Watu hao walikamatwa katika eneo la eldoret mwaka jana ambapo kesi dhidi yao ilianza.

Cheptoo hata hivyo amechukua fursa hiyo kuwaonya wenyeji wa vihiga ambao wanajihusisha na uhalifu kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.