Jamaa anayefanana na Uhuru afutilia mbali madai kuwa alipewa gari

Netizens walibaki midomo wazi baada ya jamaa anayefanana na Uhuru Kenyatta, Michael Njogo Gitonga picha zake kuenea sana na mengi kusemwa kumhusu.

Siku chache baadaye Micheal alionekana akitia saini katika mkataba ulioonekana kama makubaliano na kampuni ya maridadi Motors.

Michael ambaye alionekana ndani ya gari la aina ya Lexus LX570 2016 ambayo ina gharimu millioni 15, haijabainika kwanini fununu wala kampeni kuwa Michael alipewa gari hilo kama zawadi.

Baada ya pcha hizo kuenea Michael alijitokeza na kusema,

"Hii story watu wanasema kuwa nimepewa gari hilo ni uongo mtupu, niko kwa nyumba yangu huku nikifanya mazoezi ya kutotangamana na watu na nikidumisha usafi

Watu wanapaswa kuacha uongo na kusema ukweli mimi ndio Michael Gitonga Njogo." Alizungumza Michael.

Je ukweli ni upi na ni nani anasema ukweli swali ambalo limesalia akilini mwa Wakenya wengi.