Jamaa ashtakiwa kwa kumchapa aliyekuwa mpenzi wake

kibera
kibera
Mwanaume mmoja siku ya Alhamisi, alishtakiwa kwa kosa la kumchapa aliyekuwa mpenzi wake kwa kuanza uhusiano wa kimapenzi na mpenzi mwingine bila kumjuza.

Martin Imbukule alikuwa amekaa na mpenzi wake Trizah Wanjiku kwa miaka miwili kisha wakaamua kukata ushirikiano wao mwezi wa saba mwaka huu.

Siku chache baada ya wapenzi hawa kuachana, Martin alimuona Trizah na rafiki zake, kisha akaamua kumfukuza, kumkamata na kumpiga.

Zaidi ya hayo, Trizah alisema kuwa, Martin alimtusi sana akamwita malaya na kumjeruhi uso.

"He abused me that I was a prostitute and a woman who always sleeps around with desperate men," Wanjiku told police.

Trizah aliokolewa na wapita njia baada ya rafiki zake kumtoroka Martin Imbukule aliyekuwa na hasira kibao.

Martin Imbukule alienda mbekle ya korti ya Kibera na kuhukumiwa na hakimu Joyce Gandani.

Licha ya hayo, Jamaa huyu, aliachiliwa kwa dhamana ya shilingi 30,000.

Kesi hii itasikizwa Tarehe ishirini na sita mwezi wa 7.

Ama kwa hakika, mapenzi yana mambo!