Jamaa atiwa mbaroni kwa wizi wa Ng'ombe Shinyalu - Kakamega

EYCHd6BWoAUcZ1o
EYCHd6BWoAUcZ1o
Jamaa mmoja kutoka eneobunge la Shinyalu kaunti ya Kakamega ametiwa mbaroni baada ya kupatikana na ng'ombe wa wizi. Inadaiwa kuwa mshukiwa huyo alikuwa amebadili chumba chake cha kulalal kama kichinjio cha ng'ombe wa kuibwa.

Maandamano yameshuhudiwa katika mji mkuu wa Harare Zimbabwe baada ya viongozi wa chama cha upinzani cha MDC watatu kupotea katika njia ya kutatanisha.

Ubalozi wa Uingereza katika taifa hilo umeelezea masikitiko yake kuhusiana na dhulma wanazopitia viongozi wa upinzani Zimbabwe wakishtumu uongozi wa rais Mnangagwa kwa kuwanyanyasa viongozi hao.

Yanajiri hayo huku shirika la afya duniani WHO likitaka taifa jirani la Burundi kuelezea ni kwa nini liliamua kuwatimua maafisa wa WHO wanaohudumu katika taifa hilo.