Jamaa aumia vibaya katika ajali kwenye barabara ya Waiyaki

IMG-20200223-WA0006
IMG-20200223-WA0006

Jamaa mmoja aliumia vibaya baada ya gari kumgonga kabla ya kutoweka katika barabara ya Waiyaki way, jumapili.

Kumekuwa na msongamano wa magari katika barabara hiyo, karibu na daraja la St Mark's.

Inasemekana dereva huyo alijipeleka mwenyewe hadi kituo cha polisi cha Parklands ili kuandikisha taarifa.

Mashahidi wanasema kuwa Jamaa huyo alikuwa hapo kwa mda wa masaa mawili na iliwabidi wafunge barabara ili aweze kuhudumiwa.

Jamaa huyo alikuwa akivuka barabara na mguu wake uliumia vibaya. Hawezi zungumza na Inasemekana hana uwezo wa kuskia wala kuzungumza.

Mhudumu wa bodaboda alisema kuwa hawawezi mkimbiza hospitalini kwa hofu kuwa wataandikisha taarifa.