Jamaa kapatwa na mama mkwe lodging –Ungefanya nini?

Masaibu yaliyompata  Sylvanus  yamekataa kumtoka fikrani kwa sababu hatua ya kupatiakana na mama mkwe akitoka  kwenye danguro moja akiwa na mwanamke mwingine ,limemfanya kuogopa kurejea nyumbani .

Yote yalianza wakati Sylvanus na  rafiki zake walipopiga safari ya kwenda kujivinjari  katika mji wa Kimana karibu na mpaka wa kenya na Tanzania . katika eneo walikokuwa wakilewa , kulikuwa na hoteli yenye madanguro na wakianza safari yao  walikuwa wameandamana na wanadada kadhaa wa kuwapa raha . Sadfa ambayo hakujua itampata ni kwamba mama mke wake na wanawake kadhaa walikuwa safarini kwenda Kajiado  kwa mafunzo kuhusu mradi wa kilimo cha samaki na walikuwa wameelekezwa katika hoteli hiyo ili kulala kwa usiku huo kisha kesho yake warejee tena kwa mafunzo.

Bila kujua yanayomgojea  Sylvanus alipanda juu katika ghorofa kwenye chumba chake cha kulala akiwa ameandamana na msichana  wa kumpa raha usiku huo . Ilipofika mwendo was  saa  moja jioni alishuka chini akiwa na yule mwanadada amempakata wakishuka kwenye stairs ,  kwa sababu ya  ulevi wake hakugundua kwamba kulikuwa na watu waliokuwa  wakielekea katika vtumba vya kulala vilivyokuwa juu , Alipojaribu kuinua kichwa chake kuangalia mbele , Sylvanus Nusra  azirai alimuona mama mkwe wake .

Alikuwa miongoni mwa wanawake waliokuwa wanaingia katika vhyumba vya kulala ili  kesho yake waendelee na shughuli zao za masomo katika kaunti ya Kajiado . Alijaribu kurejea juu akipanda lakini  watu  wengine kadhaa walikuwa  wakishuka na hangeweza kupita . Mama mke alimuita kwa jina kwa nguvu huku bila kusita akijipata ameitikia . kwa sababu yule mwanamke aliyekuwa naye alikuwa amelewa , hakuwa na ustaarabu wa kujua kwamba Sylvanus alikuwa mashakani na aliendelea  kumshika mkono huku akimpapansa akimuambia waende nje ambako rafiki zake walikuwa wamepiga kambi

Mama mkwe aliyeonekana kuhamakishwa na  vitendo vyake alionekana kumuashiria kwa hamaki aondoke ,akiwa hataki kumuona .Sylvanus anasema pombe iliyokuwa akilini mwake ilimtoka papo hapo huku akipatwa na wasi wasi kuhusu kitakachofuata kwani alikuwa na uhakika kwamba mama mkwe wake angempigia simu binti yake na kumeueeza alikomwona Sylvanus .

Wikendi hiyo  Sylvanus alishindwa kupata  nguvu za kurejea   kwake ,alielekea kwa rafiki yake mmoja ambaye walikuwa wamekwenda  naye kwa wikendi hiyo ya raha katika sehemu ambayo hawakutaraji watapatana na mtu anayewafahamu na wa mwisho waliyewahi kufikiria wangekutana naye katika eneo hilo ni mama mkwe wake !