Jamaa katoroka na mamake wa kambo na kumuacha babake hoi

Tala man
Tala man
Wakati mwingine  ,adhabu huja kupitia njia mbali mbali na hakuna kichungvu kama adhab ya  mzee mmoja huko  Tala mabaye mtoto wake wa kiume alitoroka na mke wake-mamake wa kambo .

Justus  Nzioka  aliamua kupata mke wa pili ambaye ni wa umri mdogo  na mtu wa mwisho sana katika fikra zake ambaye angwahi kufikiria anaweza kutorokana mke wake ni mwanae mkubwa ambaye pamoja na wenzake walikuwa na hamaki sana wakati baba yao alipooa mke wa pili .  Baada ya mhemko uliotokana na  hatua ya Nzioka kuoa mke huyo ambaye alifaa kuwa rifa la watoto wake wa mke wa kwanza ,kila jambo lilitulia kumbe kulikuwa na kingine kilichokuwa kikitokota

Mtoto wake Nzioka aliyekuwa akifanya kazi Makindu kama afisa wa afya alihamishwa na kupiga kambi pale Tala ambapo alitangamana kila wakati na mamake wa kambo .Kimoja kilizaa cha pili na mtu na mamake wa kambo wakaanza uhusiano ambao haukuwa halali . Ingekuaje sasa mama wa kambo tena ajihusishe na  uhusiano na mwanawe wa kambo? Hilo halikuwakomesha kuendelea na mipango yao kwani mtoto wake Nzioka baada ya kutafakari hatua anayoeza kuchukua aliamua kumuacha baba yake hoi –kwa kukwepa na mamake wa kambo hadi Mombasa!

Wote walioijua familia  hiyo walipatwa na butwa kuhusu matukio hayo kwani mke huyo wa babake hakuwa hata ameishi naye kwa miaka miwili . Ingawaje palikuwa na uvumi kwamba mzee alikuwa kaishiwa nguvu na huenda wahudumu wa boda boda walikuwa wakimsaidia ‘kulima shamba’ hakuna aliyewahi kufikiria kwamba ni mtoto wake ndiye aliyekuwa akimsaidia babake kumridhisha mkewe .

Tatizo ni kwamba Mzee alikuwa amemfungulia mke wake wa pili hoteli katika mji wa Tala na kumuach make wake wa kwanza mashambani akiteseka . Hilo lilizua sana  lalama na kuleta uhasama miongoni mwa watu wa familia kwa mzee kwa sababu ilionekana amemteekeza mke wa kwanza kwa sababu ya mapenzi yake  mapya kwa mke wake wa pili na aliyekuwa mdogo kwa umri .

Wakati mtoto  wake  alipoamua kumtorosha mamake wa kambo na kwenda naye Mombasa ,Mzee  Nzioka hakuwa na budi ila kurudi  katika mke wa kwanza na hapo sasa ndimi zikatulia huku watu wengi wakisema ni adhabu kutoka kwa mola kwa sababu mzee alikuwa amemtenga mke wake kwa sababu ya mke wa pili ambaye sasa alikuwa ametoroka na mwanae .

Kisichojulikana hadi sasa ni  iwapo mtoto wa Nzioka waliwahi kurudi Tala kama  mume na mke hasa ikizingatiwa  kwamba mke huyo alikuwa ni wa babake. Dunia ina mambo