Polisi wanachunguza kisa ambacho mwanamume mmoja aliaga dunia kwa kuteketea ndani ya gari lake mtaani Buruburu, Nairobi siku ya Jumanne .
Walinzi wa kibinafsi waliokuwa zamuni katika nyumba za Mai Mahiu Court katika barabara ya Katulo waliliona gari hilo likiteketea katika eneo la maegesho.
Wazima moto kutoka kaunti ya Nairobi walikimbia kuuzima moto katika gari hilo aina ya Subaru Impreza nambari ya usajili KBY 779M.
Baada ya kukaguliwa mwili wa mtu huyo uliokuwa umechomeka ulipatikana na baadaye kutambukiwa kuwa wa mwanamume Terance Korir mwenye umri wa miaka 36 anayeaminika kuwa mmiliki wa gari hilo.
Marehemu alikuwa akielekeea kazini mwendo wa saa mbili unusu asubuhi wakati wa tukio hilo. Kuna madai kwamba huenda moto huo ulianzishwa na kitakasio lakini hilo halijathibitishwa. Mwathiriwa amewaacha mkewe na watoto wawiliKO.
MHARIRI: DAVIS OJIAMBO