'Jamaa wa bodaboda aliniseti kuwa nahanya,' Rose asimulia

Je ushawahi kuwa na mpango wa kando? Na je uliwahi patikana, na kama kisanga kama hicho kimewahi kupata nini kilitokea.

Mwanadada kwa jina Rose alisimulia kuwa alikuwa na mpango wa kando kwa mda wa miaka miwili na cha kuchekesha ni kuwa aliyepasua mbarika ni jamaa wa bodaboda.

Kulingana na bi Rose, aliamua kutafuta mpango wa kando pindi tu alipogundua mumewe ana hanya hanya. Lengo lake lilikuwa apate jamaa halafu wakimalizana arudi kwa ndoa yake.

Hata hivyo, uhusiano wao uliendelea na kabla ajue miaka miwili ilikuwa imeisha. Alisimulia kuwa jamaa wa bodaboda ambaye anajua wana ndoa hao wawili ndiye aliyetobolea mumewe siri.

Soma usimulizi wake,

Nilipatikana live live! Ni mtu wa boda aliniseti na si eti ni ile huwa anaskia, alikuja na akanipata live.

Hata sikutumia bodaboda ni vile ananijua na anajua bwanangu, sasa tulikuja tukaelewana na mambo yako salama sasa kwani pia yeye aliogopa.

Jamaa alianza kuhanya na nikampata si eti niliambiwa akikuja kwa nyumba anapiga mgongo kwa ukuta akilia amechoka. Massawe akaanza kuja na 600 kwa nyumba na ni mtu alikuwa anakuja na 3,000 kwa siku.

Hapo nikaanza kumshuku nikapeleleza polepole nikampata na nikashikana na mjamaa fulani. Huyo jamaa alikuwa serious alikuwa anataka kunioa na mimi ilikuwa tu revenge na nirudi kwa nyumba yangu.

Tulienda enda na yeye karibu miaka miwili na nikapatwa, bwanangu alimuongelesha na akamwambia kuwa mimi ni mke wake na amelipa mahari. Tangia hapo hajawahi taja chochote kuhusiana na hilo baada ya kunisamehe na yeye pia aliwacha kuhanya.