Jamaa watatu wakamatwa kwa tuhuma ya wizi wa magari

tao
tao
Polisi wame wakamata watu watatu ambao wanadaiwa kushirikiana kuiba gari huko mjini Eldoret. Hii ni baada ya ongezeko la visa vya wizi wa magari mjini humo.

Kamishna wa kaunti ya Uasin Gishu Johnstone Ipara, alisema kuwa bado wanawatafuta watuhumiwa wengine kadhaa ambao wanadaiwa kuhusika katika kushiriki kuiba magari katika eneo hilo.

Zaidi ya magari 300 yameibiwa katika mji huo, tukio ambalo limezua hofu miongoni mwa wamiliki wa gari ambao sasa wanaogopa kuegesha magari yao ndani ya mitaa hizo mjini Eldoret.

Hayo yakijiri, Gavana wa Taita Taveta Granton Samboja amemsuta naibu wa rais William Ruto kwa kile anasema ni kuingilia uongozi wa kaunti hiyo na kumtaka kukoma kuingiza siasa katikaswala la mzozo wa bajeti unaoendelea.

Samboja amesisitiza kuwa ni sharti kaunti hiyo ivunjwe ili kusuluhisha mzozo kati yake na wawakilishi wadi.
Awali Ruto alikuwa amemtaka Samboja kufanya mazungumzo na wawakilishi wadi.