Jamani Diamond! Staa Platnumz achangia vilivyo ndoa kuvunjika

Diamond Platnumz ameangamiza ndoa nyingine tena.

Amini usiamini ni kama vile, binti uwe au usiwe mwanamuziki, ndoa yako au uhusiano wako unaweza didimia kama utamfanya Diamond awe rafiki yako wa ndani sana.

Hata hivyo hatuwezi mhukumu Diamond kwani mwanamuziki huyu amefaulu maishani, ana hela si kwa uchache na pia ni mchanga bado, yaaani hajazeeka hivyo basi wanawake wengi wanamtamani.

Zaidi ya hayo, kwa sababu ya uraibu wake Diamond kuwa mtu karimu na wanawake wengi kumtamani, wengi wa hawa wanawake huanza kuwashuku sana wapenzi wao na wakati mwingine kwa sababu ya kukosa uaminifu, ushirikiano unadidimia tu na mambo kuisha tu.

Binti mmoja jina lake Ruby ni mwanamuziki kutoka Tanzania alifunguka mwanzo mwisho na kusema kuwa mpenzi wake amefanya maisha yake yawe ya machungu sana kwani mpenzi wake anaonea wivu urafiki wake na Diamond pamoja na Juma Jux.

Hivyo basi, kidosho huyu aliamua kujiteteta kwa kuandika ujumbe mrefu kwenye mtandao wa kijamii ili aweze kuokoa maisha yake na ya mtoto wake.

Huu ndio ujumbe wake Ruby kwenye mtandao wa  kijamii wa Instagram.

''Nimekuwa nikijiuliza niseme ama nionge kwa nani ila katika hizi dhama lazima kusema ukweli wenda nayopitia ama niliomaliza kupitia yanampata binti wa kike mwenye umri kama wangu au zaidi yangu ila tu amekuwa kifungoni kwa kasumba yakuonekana mbaya kama taswira ilivyo kwa watu wengi kuwa wanawake huwa tunazingua sana.

Nimepitia vipigo, manyanyaso, fedhea, kudhalilushwa na kuitwa majina yote kutoka katika kinywa na mikono ya mwanaume ambae alikuja kwangu kutaka support ya kimuziki ila unajua tena love doesn’t ask why? Nilijitolea kumpa support na kuonesha uma kuwa Nina muamini na Nina imani na kipaji chake ila ili hali kuna msemo unasema mwana kulitaka mwana kulipewa; Nimekuwa nikitumia ata jina langu ili dogo kumpambania na kumtambulisha kwa wasanii waliondelea ila mwisho wa siku Nimekuwa nikiambulia vipigo na kuitwa majina ambayo mengine siwezi yaandika kwasababu kuyasema ni kuweka kumbukizi Katika tamati ya maisha niliyomuomba Mungu anipe muongozo na anioneshe njia iliyo bora zaidi.

Ukiangalia baada ya kila jambo niliamini labda yataisha na mwenzangu kubadilika ila aikuwa kama nilivyotegemea. Despite kujitoa kwa familia yangu na yake na kuwa mbele kwa kila jambo lake ata kutumia kidogo changu kumpush kwa njia tofauti ila bado aikuwa na mantiki kwake.

Mimi ni binti mdogo ambae Nina vision na maisha mbele yangu siwezi katishwa tamaa na jambo lolote linaloendelea na yanayofanywa na baba mtoto wangu kwasababu nimeamua kufikia tamati laasha ningemshauri muda huo anaotumia kuyasema ya uongo angetumia kumuombea mtoto wake akuwe katika njia zimpendezayo Mungu kwasababu kwa kumuangalia sintotaka kumpa mzigo huo kwasababu binafsi anajua nilivyopambana kwake na familia kiujumla ila kwa anayofanya nakuombea Mungu akupe amani ya Moyo.

Nimejitahidi kwa uwezo wangu kukuunganisha na kaka yangu  mwisho wa siku unishushie makofi natembea nae ukuishia apo unayasambaza na ya mtu tunae eshimiana kusema natembea nae.

Hii kama mtoto wa kike inaniharibia taswira mbele ya jamii yangu na watu wanaoniangalia kama kioo ili hali ni chuki tu na kutokujitambua kunafanya mtu anaamua kuunda na magroup kusambaza stori hizi ili nionekane mbaya.

INAENDELEA…..

https://www.instagram.com/p/B42oab7hjV8/

Maskini Diamond, ndoa zaharibika bila yeye kujua sababu za ndoa hizi kuharibika.