moi referral hospital

Jambazi aliye nusurika kutoka mikononi mwa wakazi wa Taita Taveta

Polisi huko Voi kaunti ya Taita Taveta wamemuokoa mshukiwa mmoja wa ujambazi mikononi mwa wakazi wenye ghadhabu waliokuwa wanataka kumteketeza.
Mkuu wa polisi Joseph Chesire alisema kuwa mshukiwa huyo ni jambazi sugu ambaye amekuwa akisakwa na polisi kutokana na tuhuma kadha za wizi wa kimabavu na atafikishwa mahakamani hapo kesho.
moi referral hospital
moi referral hospital voi
“Mtu huyo ni jambazi mkubwa ambaye amekuwa akitafutwa na polisi, amekuwa akiiba mifugo na kutoroka kisha kuwa danganya wananchi na wananchi wamekuwa wakilalamika,

“Kwasasa amechapwa na wananchi na yuko hospitalini na ataenda mahakamani akitoka hospitali,”Alizungumza Chesire.

Nilipe deni yangu! Gospel star Bahati exposed for being ‘selfish’ and ‘two-faced’

Kwa Sasa anapokea matibabu Katika hospitali ya rufaa ya Moi mjini humo kutokana na kipigo alichopokea kutoka kwa wakazi.

SOMA:

Wanaharakati katika kaunti ya Taita Taveta wanalalamikia kutengwa na serikali ya kaunti katika utoaji maoni kuhusu miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali.

Sababu ya kuanzisha na vile nilianzisha timu ya mpira ya Majirani FC – Majirani

Mohammed Washalla kutoka SUPKEM alisema ukosoaji mkubwa kutoka kwa wanaharakati ndio sababu kuu ya gavana Granton Sambaoja kufumbia macho maswala kadha ya utepetevu yanayoibuliwa na wakazi.
Taita-Taveta-County-Assembly-chamber
“Hatuna vita na wao wametunyima nafasi ya kutoa maoni yetu, hapa tuna ona kuna utepetevu, na wakitunyima tutaendelea na mbele na mahali kuna nafasi yetu,
“Wametunyima nafasi ya kusema mambo ambayo yanatuumiza sisi kama wananchi na sisi ndio walipa ushuru,
“Kama pesa ambayo inatoka Nairobi haitumiki sawasawa sisi ndio macho tuta toa kongole mahali tunaona huduma ni sawasawa,na mahali huduma imedorora tutasema huduma imedorora,” Walieleza wanaharakati.
Anasema wataendelea kuishinikiza serikali kutoa huduma bora.
KATIKA KAUNTI YA KAKAMEGA: Nikwamba…

Viongozi wa makanisa katika eneo la butere kaunti ya Kakamega wamelalamikia ongezeko la visa vya wizi makanisani na kuitaka idara ya usalama kuwajibikia swala hilo.

Ilikuaje: Willy Paul aeleza kwanini akaimba nyimbo za kimapenzi

“Hata sisi siku hizi tumeshangaa sana kuona watu hawana uoga na kuimba kanisani na kuiba vyombo vya mchungaji,
“Pia kule mahene walikuwa wameiba mwaka jana inaonekana kukosa na hawana heshima na vyombo vya kanisani na mali ya mwenyezi Mungu,” Alieleza Askofu.
Wakiongozwa na askofu wa kanisa la ki angilikana jimbo la Butere Tim Wambunya wamesema wizi makanisani unashuhudiwa kwa kiwango cha juu huku wahusika wakikosa kukamatwa.

Photo Credits: file

Read More:

Comments

comments